Mahusiano na ndoa

Njia za Kumtuliza Mwanaume na Kudumisha Amani na Furaha Ndani ya Mahusiano




Njia za kumroga mwanaume atulie kwenye mahusiano.


Ni ndoto ya kila mmoja kuona ndoa yake inakuwa na amani na
furaha huku uaminifu ukiwa ndio mzizi wake. Dhana nyingi huelezea kuwa mwanaume
ndio huwa msaliti mkubwa linapokuja suala la mahusiano. Lakini dhana kama hiyo
si sahihi, kwani usaliti ni hulka ya mtu husika. Lakini pia kwa asilimia kubwa,
usaliti huwa unachangiwa na watu wenyewe walio katika mahusiano. Ewe mwanamke,
fuata hatua zifuatazo ili kumtuliza mwanaume wako:


●    IBADA NA DUA

Jamii nyingi hasa za kiafrika huwa na imani
juu ya uwepo wa muumbaji wa mbingu na nchi. Huamini kuwa, hakuna kitu
kilichokuwepo duniani bali kililetwa na mungu. Pia huamini kuwa mungu ndo kila
kitu na kwake hakuna jambo lolote linaloshindikana. Akisema jambo liwe, nalo
huwa kama alivyoliamrisha. Ikiwa wewe ni mtu wa imani juu ya uwepo wa mungu,
tumia muda wako kumuomba kwa sala na maombi aweke amani katika ndoa yako.
Mtangulize mungu wako katika kila jambo utakalokuwa unalifanya. Muombe
amuongoze mumeo awe kipofu katika kuangalia wanawake wengine kinyume na sheria
alizoweka Mungu. Muombe amuepushie mumeo vishawishi vya shetani juu ya
kuangalia na kutamani visivyo halali kwake. Wanawake wengi ukimkuta anamuombea
dua mumewe, huwa wanaomba apate mali nyingi tu kwa sababu hakuna anayetaka
kuishi katika umaskini huku wakisahau kuwa amani na uaminifu katika ndoa ni
utajiri mkubwa zaidi.

●    CHAKULA

Kiuhalisia, hakuna binadamu asiyependa kula
chakula kizuri. Mwanaume hufurahi zaidi anapokula chakula kilichokuwa kitamu tena
kilichopikwa na mwanamke wake. Ewe mwanamke, jitahidi chakula anachokula mwanaume
wako, uwe unampikia wewe. Pia usione haya kuulizia au kujifunza mapishi kutoka kwa
watu wengine pale unapohisi aina fulani ya chakula ambayo mumeo huwa anaipenda zaidi
kwako ni mtihani kupika. Kama unayapenda mahusiano yako, usipendelee kumuachia binti
wa kazi apike chakula kwa ajili ya mumeo. Kwa sababu huwezi kujua kesho yako.

●     USAFI

Mwanaume anapenda kupendeza. Anapenda mazingira
ya nyumbani kwake yawe safi muda wote. Na wewe mwanamke ni moja ya hayo mazingira.
Hakikisha unakuwa msafi. Sio unashinda na chupi moja kuanzia asubuhi mpaka usiku.
Ukioga usiku mpaka usiku. Huo ni uchafu kwa mtoto wa kike. Hakikisha angalau chupi
yako unabadilisha mara tatu kwa siku. Fanya usafi wa mwili wako hata kama ni mara
tatu ikibidi hasa pale mwanaume wako anapokuwepo siku kama za mwisho wa juma. Sio
unakaa na mtu, ananuka jasho hata mbuzi haoni ndani. Pia hakikisha unapoenda kuoga
unasafisha tunda vizuri, na sio kuoga dakika tano, tena eti mwanamke anaoga akiwa
amesimama mpaka anamaliza. Huo ni uchafu. Mwanamke lazima uchuchumae ili maji yapite
vizuri sehemu zilizojificha. Hakikisha nywele ya sehemu za siri zinanyolewa na sio
mtu akitaka kupita akutane na msitu mpaka aogope. Uchafu ndo huwakimbiza mwanaume
wengi na kukimbilia wanawake wa nje ambao hawaoni shida kuoga mara kumi kwa siku
kwa sababu huwahitaji mwanaume wa watu.

●    ADABU

Kuna watu hutumia akili nyingi sana kuhakikisha
wanapata riziki yao. Lakipi pia wapo ambao hutumia nguvu nyingi kuhakikisha wanapata
riziki yao. Ewe mwanamke, jitahidi kuwa na adabu kwa mwanaume wako. Usibishane nae
kwa maneno makali. Akitoka kazini, mpokee hata kama ana mfuko mdogo mkononi mwake.
Kuna wakati mwanaume anaharibu kazi yake kwa sababu ya maneno makali kutoka kwa
mwanamke wake. Faraja ambayo mwanaume anaweza kuipata kutoka kwa mwanamke, huwa
ni tiba ya akili ya mwanaume, kwa sababu pia inaweza kumsaidia kupata mawazo mapya
ya kutatua changamoto ya maisha ambayo ilimshinda kuitatua kwa haraka.

●     UAMINIFU

Mwanaume anapenda mwanamke ambaye anajitambua
na ambaye ni muaminifu kwenye suala la mahusiano na mali za mwanaume. Usipokuwa
muaminifu, ni rahisi sana kumfanya mwanaume wako kutafuta mwanamke mwengine na kukusaliti.

Uongo usiokuwa na faida, ni sumu ya mapenzi.


●      KUJIHESHIMU

Hapa wanawake wengi, hasa waliozaliwa katika
karne ya 21 huwa ni suala gumu kwao. Moyo wa mwanaume una sehemu mbili, sehemu ya
kwanza ni kutamani na sehemu ya pili ni kupenda. Mara nyingi mwanaume hutamani kutokana
na kile anachokiona. Suala la kupenda hutegemea katika kujiheshimu kwa mwanamke
husika. Mwanaume anapenda mwanamke anayemmiliki awe anajiheshimu kwa mavazi na matendo
yake katika jamii. Hakuna mwanaume anayependelea kumuona mwanamke anayempenda akiwa
amekaa vijiweni na kundi la wanaume. Pia hakuna mwanaume anayependa mtu anayempenda
akiwa amevaa nusu utupu na kujiposti posti katika mitandao ya kijamii. Ukiona mwanaume
wako yupo hivyo, dada yangu unapaswa kujua kuwa hapo unatumika tu na mahusiano yenu
hayawezi kudumu.

●     TENDO LA NDOA

Sababu kubwa inayowafanya watu kuingia katika
mahusiano ni hiki kitu. Tendo la ndoa ndo shina kama sio mzizi wa mahusiano. Hiki
kitu ndo kinasababisha mtu kuonekana msaliti wa mahusiano, hiki pia ndicho kinasababisha
mapenzi kukolea. Usipokuwa makini na hiki kitu, ni rahisi sana kusalitiwa. Ewe mwanamke,
unatakiwa kujua kuhusu tendo la ndoa. Usione aibu kujifunza. Jifunze sehemu muhimu
unazotakiwa umshike mwanaume, jifunze  vitu
gani ambavyo unapaswa umfanyie mwanaume kabla ya tendo la ndoa. Huwezi kumchinja
kuku kabla ya kumuandaa. Hivyo ndivyo ilivyo, kama wewe unavyopenda kuandaliwa kabla
ya tendo la ndoa, ndivyo hivyo na mwanaume anavyopenda kuandaliwa kabla ya tendo
la ndoa. Tafuta mbinu za kumuandaa mwanaume wako.

Pia hakuna mwanaume anayependa mwanamke mvivu
katika suala la tendo la ndoa. Kama hujui chochote kuhusu mapenzi, jifunze unatakiwa
kufanya nini wakati wa tendo la ndoa. Jifunze mitindo ambayo itakufanya uonekane
kuwa wewe sio mvivu. Sio unakaa tu kitandani, ukilalishwa ndo umelala utafikiri
mbuzi anasubiri kuchunwa. Ewe mwanamke, ukiwa hivyo, kila mwanaume utamuona hana
nguvu za kiume kwa sababu huwezi kupigana vita na mtu ambaye harudishi majibu. Ili
vita iwe ya muda mrefu, lazima anayepigwa nae, arudishe majibu. Mwanamke wewe, usitegemee
kuridhishwa ikiwa haujitumi kitandani. Unaonaje kwenye mechi ya mpira wa miguu,
ikiwa timu moja inajituma na kushambulia sana na nyengine haijitumi kabisa, timu
ipi itapata magoli mengi, na unatakiwa ujue kuwa magoli yakishakuwa mengi, hata
morari huisha pia. Kauli yake itakuwa moja tu, ngoja nimalize niondoke.

Jifunze kukata kiuno, jifunze kukuna nazi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *